ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ZOEZI LA UPIMAJI WA MARADHI YA MOYO LAANZA MKOANI ARUSHA

Na Vero Ignatus, Arusha
Imeelezwa kuwa 75%ya vifo vinavyotokea katika mataifa yanayoendelea ukanda wa Afrika ikiwemo Tanzania vinasababishwa na magonjwa yasiyoambukizwa kwa utafiti uliofanywa 2012 na shirika WHO.
Hayo yamesemwa na Dkt Bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya inayojihusisha na magonjwa ya moyo ya JKCIA Dkt Samwel Rweyemamu katika Uzinduzi wa zoezi la upimaji wa maradhi ya moyo mkoani Arusha.

Amesema kuwa kutokana na takwimu zilizofanywa 2016 wilayani simanjiro mkoa wa Manyara zinaonyesha kuwa 30%ya wanaume wote waligundulika kuwa na shinikizo la damu, hiyo ikiwa ni data zinazofanana za watu wanaoishi mjini.
 
'' Data zinaonyesha tukiweza kupambana shinikizo la damu, uzito uliokithiri, kuangalia sukari kwenye miili yetu na kupima mafuta kwenye mwili tutapunguza vifo kwa 80% '' alisema Dkt Rweyemamu

Kwa upande wa mwenyekiti wa Bodi Balozi Dkt. Ladis Komba amesema kuwa azma la AICC katika eneo la Afya lina shabiana na azma ya serikali katika kusogeza huduma bora kwa wan... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More