ZOEZI LA USAJILI WA WATUMIAJI HUDUMA YA MAJI BILA KIBALI LAANZA DAR NA PWANI - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

ZOEZI LA USAJILI WA WATUMIAJI HUDUMA YA MAJI BILA KIBALI LAANZA DAR NA PWANI

Shirika la MajiSafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Miji ya Bagamoyo na Kibaha Mkoani Pwani kuwa zoezi la usajili kwa waliojiunganishia huduma ya Maji bila kibali cha shirika limeanza rasmi kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Agosti mpaka Septemba, 2018.
Hivyo wananchi ambao wamejiunganishia huduma ya Maji bila kibali, shirika linawataka kufika katika Ofisi yoyote ya Dawasco iliyo karibu kwa ajili ya kusajiliwa na usajili utafanyika bure bila faini yoyote kwa kipindi hichi.
Aidha baada ya zoezi la usajili kukamilika kutakuwa na msako mkali wa nyumba kwa nyumba na wananchi watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE).Copyright 2007-2017 @KAJUNASON BLOG... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More