Zungu la dawa za kulevya duniani ‘El Chapo’ ahamishiwa gereza lingine hatari zaidi Marekani, Hofu yatawala - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Zungu la dawa za kulevya duniani ‘El Chapo’ ahamishiwa gereza lingine hatari zaidi Marekani, Hofu yatawala

Gwiji la mtandao wa biashara za madawa ya kulevya duniani,  Joaquin Guzman almaarufu kwa jina la El Chapo amehamishiwa gereza lingine lenye ulinzi mkali zaidi nchini Marekani la ADX Florence la mjini Colorado.Guzman alihukumiwa kifungo cha maisha jela na miaka mingine 30 siku ya Jumatano ya wiki hii baada kukutwa na makosa ya biashara ya dawa za kulevya na kushiriki njama za mauaji wakati akiwa kiongozi wa genge kubwa zaidi la biashara hiyo la Sinaloa.


Taasisi inayosimamia magereza nchini Marekani (MCC) imethibitisha taarifa hiyo, Na kueleza kuwa ni kutokana na rekodi mbaya ya kutoroka magerezani kwa mfungwa huyo.


El Chapo (62) aliwahi kutoroka mara mbili kwenye magereza yenye ulinzi mkali nchini Mexico mwaka 2001 na 2015, Kabla ya kukamatwa tena mwaka 2017.


Gereza la ADX Florence lina wafungwa 375 na lilifunguliwa mwaka 1994. Imeelezwa kluwa ndio gereza linalofungwa watukukutu wote wanaoisumbua Marekani na dunia kwa ujumla, Na hakuna mfungwa aliyewahi kutoroka.


Hukumu ya kesi hiyo ... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More